BI KIDUDE AFARIKI DUNIA
BI KIDUDE ENZI ZA UHAI WAKE
Mwanamuziki nguli wa tanzania na Afrika mashariki Fatma Baraka Hamisi
ali maarufu kama bi Kidude amefariki dunia jana tarehe 17/04/2013
majira ya saa sita mchana akiwa nyumbani kwa ndugu zake nje kidogo ya
mji wa unguja, bi kidude amefariki dunia akiwa na umri zaidi ya miaka
100 alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kisukari na uvimbe uliokuwa
kwenye kongosho.
Safari ya maisha ya muziki wa bi kidude ilianza tangu akiwa na umri wa
miaka 10 alianza kwa kupiga ngoma za unyago na kuimba,baadaye alianza
kuimba muziki wa Pwani maarufu kama taarabu ambao ni muziki uliompa
umaarufu mkubwa Tanzania na hata nje ya nchi kutokana na umaarufu huo
alipata fursa ya kutembelea nchi kama vile Oman,Ufarasa, Uingereza na
nyingine nyingi.
Muda mwingi alifanya muziki akiwa kwenye ziara za kuzunguka nchi za nje
na alipofikisha takribani umri wa miaka 40 alirudi kufanya muziki
nyumbani kwao Unguja hata hivyo kuna baadhi ya nyimbo zilizompa umaarufu
mkubwa ni kama vile muogo wa jang'ombe,yalaiti na nyingine nyingi
lakini katika maisha yake hakubahatika kuzaa mtoto pia bi kidude alipata
elimu ya korohani tu hakubahatika kusoma elimu ya dunia.
Bi kidude amezikwa leo tarehe 18/04/2013 kijijini kwao huko unguja.
Mungu ailaze roho ya marehemu Fatma Baraka Hamisi (bi kidude) mahali pema peponi.
Amina
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni