Jumla ya Mara Iliyotazamwa

Alhamisi, 18 Aprili 2013

KURASA ZA MWANZO NA MWISHO ZA MAGAZETI YA APRIL 18 2013

Posted: 18th April 2013 by bongocarpet.blogspot,com in News
1
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
Gazeti la Mwananchi, picha inaonyesha Mbunge Lema akizuia askari wasimtoe Tundu Lissu.
Naibu Spika wa Bunge JOB NDUGAI amemtoa nje ya Bunge kwa muda wa siku tano Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni TUNDU LISSU kwa madai ya utovu wa nidhamu na kuanzisha majibizano bungeni kitendo kinachokiuka kanuni za bunge.
Wengine ambao wamepewa adhabu hiyo ya kutohudhuria vikao vya bunge kwa siku tano ni Mbunge wa Mbeya Mjini JOSEPH MBILINYI, Mbunge wa Arusha Mjini GODBLES LEMA, Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji PETER MSIGWA, Mbunge wa Nyamagana EZEKIA WENJE na Mbunge wa Ilemela HIGHNES KIWIA ambao walikuwa wakiwazuia askari wa bunge kumtoa nje LISSU.
Namkariri Naibu Spika akiongea Exclusive na bongocarpet.blogspot.com nje ya bunge akisema “nimemuonya zaidi ya mara kumi kwa jioni ya leo peke yake kwamba demokrasia ya kibunge ni ya kuwapa watu wengine nao nafasi ya kusikika, kila anaesimama anakatishwa yeye kasimama dakika zake zote amekatizwa na kina nani? kinachokosekana kwenye bunge hili ni uvumilivu wa kumsikiliza mwingine, watu wanapenda kumshambulia mwingine lakini hawako tayari kusikiliza wengine wakiwajibu, tunalaumiwa na kila mtu….. hata hatua nilizozichukua ni hatua ndogo tu”

Kabla ya uamuzi wa kutolewa nje ya Viwanja vya bunge haujatolewa, Mbunge wa Iramba Magharibi MWIGULU NCHEMBA ndiye aliyekuwa akichangia Bajeti ya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma ambapo namkariri hapa akisema “mimi ni ninachokumbuka labda watu wengine kumbukumbu sijua wanakua na hangover gani, kitu ninachokitambua kwamba Rais amekua mtu wa kwanza kukemea jambo la udini, kuna mgombea wa chama kimojawapo alikua anakwenda anaongea na baadhi ya Viongozi wa kidini kama ndio viongozi na mikutano ya ndani ya chama chake, hili linakubalika wapi? wakari CCM inatumia mabalozi, wenyeviti wa tawi…..”

Mbunge wa Longido LEKULE LAIZER ni kama ametabiri kutokea kwa jambo hilo kabla kwani wakati anachangia amepinga vitendo vya vurugu bungeni hali iliyopelekea kuwakumbuka wabunge wa zamani, namkariri akisema “hivi Mbunge mwenzako anapoongea unaanza kumzomea unafikiria nini? hatujawahi kufikia kiwango hiki”

Sekunde chache kabla ya Naibu Spika kuagiza Tundu Lissu atolewe, alisema “Mh Tundu Lissu sijui ni huu ugeni wa kuwa bungeni, ndio lazima nitoe maoni yangu kama kiongozi… unakuwa wewe ni sehemu ya kufanya vurugu ndani ya bunge? nasema hivi…. askari toa nje Tundu Lissu, askari wakwapi…. toa nje”
Wakati Naibu spika akitoa hilo agizo, wabunge wengine kadhaa walisikika wakisema…. “haiwezekani…… huo ni ubabe…. ubabe ubabe…. polisi, tutoke wote…..” 

BI KIDUDE AFARIKI DUNIA

BI KIDUDE  ENZI ZA UHAI WAKE           
Mwanamuziki nguli wa tanzania na Afrika mashariki  Fatma Baraka Hamisi ali maarufu kama bi Kidude  amefariki dunia jana tarehe 17/04/2013 majira ya saa sita mchana akiwa nyumbani kwa ndugu zake nje kidogo ya mji wa unguja, bi kidude amefariki dunia akiwa na umri zaidi ya miaka 100 alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kisukari na uvimbe uliokuwa kwenye kongosho.
Safari ya maisha ya muziki wa bi kidude ilianza tangu akiwa na umri wa miaka 10 alianza kwa kupiga ngoma za unyago na kuimba,baadaye alianza kuimba muziki wa Pwani maarufu kama taarabu ambao ni muziki uliompa umaarufu mkubwa Tanzania na hata nje ya nchi kutokana na umaarufu huo alipata fursa ya kutembelea nchi kama vile Oman,Ufarasa, Uingereza na nyingine nyingi.
Muda mwingi alifanya muziki akiwa kwenye ziara za kuzunguka nchi za nje na alipofikisha takribani umri wa miaka 40 alirudi kufanya muziki nyumbani kwao Unguja hata hivyo kuna baadhi ya nyimbo zilizompa umaarufu mkubwa ni kama vile muogo wa jang'ombe,yalaiti na nyingine nyingi lakini katika maisha yake hakubahatika kuzaa mtoto pia bi kidude alipata elimu ya korohani tu hakubahatika kusoma elimu ya dunia.
Bi kidude amezikwa leo tarehe 18/04/2013  kijijini kwao huko unguja.
Mungu ailaze roho ya marehemu Fatma Baraka Hamisi (bi kidude) mahali pema peponi. 
Amina